Klabu ya Coastal Union inatarajia kuachana na wachezaji 12 wakiwamo wanne watakaotolewa kwa mkopo ili kupisha sura mpya nane za kazi kwa ajili ya msimu ujao, huku ikieleza Wagosi hao walimaliza msimu uliopita nafasi ya 12 kwa alama 33, japokuwa hawakuwa na mwanzo mzuri hadi uongozi kufikia hatua ya kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi.

Timu hiyo ilianza msimu na kocha kutoka nchini Kenya Yusuph Chippo aliyetemwa baada ya mzunguko wa kwanza na mikoba yake kube beshwa Fikiri Fllas aliyemaliza nao Ligi Kuu.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Elias aliliambia Mwanaspou kuwa licha ya kupambana kuibakiza Ligi Kuu, lakini hakerwa kazi rahisi na kwamba ili msimu ujao isitokee presha amewasilisha ripoti yake ikihitaji maboresho.

Amesema ili kurejea kwa nguvu mpya amependekeza kuachwa wachezaji wanane, huku wanne ambao walionyesha ubora, lakini wakakosa namba watolewe kwa mkopo katika timu nyingine ili wapate uzoefu.

Nahitaji kuongeza nguvu eneo la kipa, mabeki, kiango na straika kwa sababu tuliweza kutengeneza nafasi la hakuwa makini kufunga, lazima tuje na mabadiliko makubwa ili kuendana na kasi,” amesema Elias.

Young Africans yafunguka ishu ya Cedric Kaze
CAG abaini dosari uendeshaji masoko ya Samaki