Polisi mjini New york Marekani, wanachunguza mauaji ya kasisi wa kiislamu pamoja na msaidizi wake katika eneo la Queens.

Imamu Maulama Akonjee pamoja na Tharam Uddin walipigwa risasi kichwani wakati wakielekea nyumbani mara baada ya ibaada ya maombi hapo jana.watu hao wawili walipigwa risasi na mshambuliaji aliyekuwa akiwavizia.

Imamu Maulama Akonjee, 55, alihamia New york miaka miwili iliyopita kutoka Bangladesh,baaada ya mashambulizi hayo walikimbizwa hospitalini japo  waliaga dunia muda mfupi baadaye.

Shambulizi hilo lililotokea mchana kweupe na  limeshtua jamii ya waislamu katika eneo hilo.

Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wametaja shambulizi hilo kuwa la chuki dhidi ya dini ya kiislamu, na kumlaumu mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwa kuchochea chuki dhidi ya waislamu.

Afisa wa baraza la uhusiano mwema wa Marekani na waislamu ameliambia shirika la habari la Reuters. “kuna maombolezo, na kilio kikubwa cha haki.”

Hata hivyo maafisa wa polisi wanasema kwamba bado hawajadhibitisha nia ama lengo la shambulizi hilo, na kwamba hawawezi kudhibitisha kwa uwazi kwamba waliuwawa kutokana na imani yao

Serikali Ya China Kusaidia Chuo Cha Usafirishaji NIT
Wafilipino Wakataa Rais Wa Zamani Wa Nchi Hiyo Kuzikwa Katika Makaburi Ya Mashujaa Kwa Tuhuma Za Ufisadi