Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Chuachua amesema kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwsa ajili ya hewa ya ukaa ni kupata fursa ya biashara hiyo ambayo faida yake itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wake.
Dkt. Chuachua amebainisha hayo na kusema wilaya ina fursa kubwa ya kuwekeza katika biashara hiyo kwa kuzingato kuwa kilomita za mraba 12,084.5 sawa na asilimia 86 ya eneo lote na mradi huo ni muhimu.
Amesema, “mradi huu ni muhimu kwani utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya halmashauri ambayo kwa asilimi 80 yaekuwa yakitona na mazao ya kilimo. mradi utasaidia katika kutunza mazingira ya ardhi oevu ambayo ndio chanzo cha maji katika Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema kuwa Biashara ya Kimataifa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo kuwezesha nchi wanachama kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema, mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ongezeko la joto duniani na vipndi vya baridi na mvua kupungua hali inayochangia ukame na kwamba misitu ikiwa mingi itasaidia katika kunyonya gesijoto inayochangiwa na shughuli za kibinadamu zikiwemo moshi unaotokana na magari na viwanda.