Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya Korea kwa jitihada zake za kuendelea kuiunga mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo hasa sekta ya uchumi wa buluu.

Dkt. Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya bahari ya Korea, Dk.Kim Jong-Deog aliyefika kwa mazungumzo pamoja na kumualika Kongamano kubwa la Afrika Mashariki litakakalojadili fursa na rasilimali za bahari zitakazoakisi azma ya zana nzima ya uchumi wa buluu nchini.

Alisema anaamini mkutano huo utawajengea uwezo wananchi wengi zaidi katika kujikomboa na kujifunza mengi yatakayotokana na mkutano huo na kueleza kuwa ni fursa nzuri kwa ustawi wa sekta ya uvuvi Zanzibar.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 14, 2023
Uteuzi: Lukuvi, Bulembo washauri wa Rais Siasa, uhusiano