Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, linawashikilia watuhumiwa 23 kwa makosa mbalimbali ikwemo kukutwa na Bangi Kilo tisa, lita 920 za Gongo na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo,

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo 24 Oktoba, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Katabazi amesema operesheni hiyo ni ya kuanzia Oktoba 11, 2023.

Amewataja waliokamatwa na makosa hayo ni Abdi Rajabu, Lobulu Slaa, Daudi Laizer, Laida Leheyi, Anthony Alphonce na wengine 19 na kusema katika operesheni hiyo, mali mbalimbali zilikamatwa ikiwemo Pikipiki aina ya Kinglion yenye namba za usajili MC 174 CZX.

Vingine vilivyokamatwa ni simu sita, TV mbili, Magodoro sita na noti za fedha za kigeni huku akisema operesheni hiyo ni endelevu na kuwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika Jeshi hilo, ili kuzuia na kutokomeza uhalifu katika Mkoa huo.

Singida FG yaisubiri Young Africans Dar
Jose Mourinho alalamikia kadi nyekundu