Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Nchini Tanzania – TAOMAC, kimekanusha taarifa za uvumi zinazosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, zinazodai kuwa wamekaa kwenye kikao na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA na kuishia kwenye mtafaruku na kutokuelewana katika kikao hicho.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi, TAOMAC pia imesema kwa niaba ya wanachama wao ambao wanajumuisha zaidi ya asilimia 97 ya soko la mafuta yanayoingizwa nchini, wanakanusha taarifa hizi kwa kuwa sio za kweli.

Aidha, sehemu ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, “Hatujaakaa kikao na EWURA kwa zaidi ya wiki mbili. Pia hatujawahi kukaa kikao na EWURA na kuishia kwenye mtafaruku. Aidha, sekta ya uagizaji na usambazaji wa mafuta inapitia changamoto ya ukosefu wa dola.”

“Lakini tumeshakaa vikao na mamlaka zinazohusika na tumeahidiwa kuwa tatizo hili linafanyiwa ufumbuzi. Wanachama wetu wanaendelea kuagiza mafuta na wataendelea kufanya hivyo, ili kuhakikisha nchi haikosi mafuta,” Imefafanua taarifa ya TAOMAC.

Sisi tulitoa tahadhari, hatuwazuii - Dkt. Chandika
Jengeni hoja acheni kejeli - Kinana