Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi wa fani mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, uboreshwaji wa miundombinu, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DkT. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo hii leo akifungua Kongamano la nane la Wahandisi Wanawake Tanzania – TAWECE, lililofanyika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wahandisi hasa Wanawake na mafundi sanifu.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali itahakikisha inawasaidia Wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu ya Sekondari, Vyuo vya mafunzo ya amali na Vyuo Vikuu katika hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake nchini.