Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Utatu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika – SADC, uliofanyika kwa mtandao.

Balozi Shelukindo, ameshiriki katika Mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa DRC.

Aidha, Mkutano huo pia ulifuatiwa na Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC MCO), ambapo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax.

Dkt. Tax aliongoza ujumbe huo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.

Makala: Mlima Hanang' ulivyobeba siri ya Warbabaig kiutalii
Bosi Simba SC aitumia salamu Al Ahly