Kenya watu 24 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya wizi wa fedha takriban Dola za Marekani milioni 100 za Shirika la Vijana la Huduma ya Taifa (NYS).
Ambapo watu hao wamewekwa rumande kwa kipindi cha wiki moja kupisha upelelezi wa kina kufanyika dhidi ya tuhuma inayowakabili.
Hata hivyo Jaji ameamrisha watuhumiwa hao kukaa rumande mpaka pale uamuzi wa kuachiliwa kwa dhamana utakapofanyika Jumatatu ya wiki ijayo.
Miongoni mwa walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia, Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai, vyanzo vya habari vimeripoti Jumatano.
Mapema Jumatatu wiki hii vyombo vya usalama nchini Kenya vilimtia nguvuni Ndubai ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa wizi.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai amsema watu 17 walikuwa wanashikiliwa na polisi.
Aidha, Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao Kenya wameipongeza serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kwa hatua iliyochukua dhidi ya ufisadi.
Katika tamko la pamoja ikiwemo Marekani na Uingereza, wameeleza kuwa watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua, ikiwemo kutaifishwa mali zao zinazotokana na ufisadi.