Ufaransa imesema imepata vitisho vya kuwepo kwa mabomu sehemu mbalimbali na kupelekea mamlaka za usalama kuvifunga Viwanja vya ndege 12 pamoja na Ikulu ya Versailles.

Waziri wa sheria wa Ufaransa, Éric Dupond-Moretti amesema miongoni mwa waliotoa taarifa hizo ni Vijana wadogo wasiowajibika na kwamba wazazi wao watalazimika kulipia hasara inayotokana na vitisho hivyo.

Amesema jambo hilo halikubaliki na kwamba kuzusha hali ya hofu isiyohitajika nchini humo ni kulitia Taifa hasara kwani kufunga Viwanja hivyo kunazuia uingiaji wa mapato na biashara.

Vitisho vya mabomu vimeongezeka nchini Ufaransa na hivi karibuni imetangazwa kuwepo kwa kiwango cha juu zaidi cha tahadhari ya matendo ya kigaidi.

Manchester United kumkosa Casemiro
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 21, 2023