Uongozi wa Simba SC upo katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi juu ya hatina ya Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji, Jose Luis Miquissone ambaye amekuwa na changamoto ya kucheza tangu ajiunge na timu hiyo, mwanzoni mwa msimu huu 2023/24.
Luis ni kati ya wachezaji waliosajiliwa kwa mbwembwe katika msimu huu, ambaye alikuja kwa ajili ya kuiboresha safu ya kiungo cha ushambuliaji ndani ya Simba SC akitokea Al Ahly ya Misri.
Simba SC ipo katika mipango ya kuboresha kikosi chake kwa kuingiza maingizo mapya na kuachana na wachezaji wengine ambao wameshindwa kuonyesha ushindani katika kikosi cha kwanza.
Mmoja wa Mabosi wa timu hiyo, mwenye ushawishi wa usajili amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo, iliyopo chini ya Mwenyekiti wa Bodi, Abdallah Salim “Try Again’ inafikilia kuachana na kiungo huyo katika Dirisha Dogo lililofunguliwa Juma lililopita.
Bosi huyo amesema kuwa ukubwa wa mkataba wa miaka miwili ndiyo unawapa ugumu wa kuuvunja, ili waachane na aende akatafute changamoto nyingine ya ushindani.
Ameongeza kuwa wakati viongozi hao wakifikilia kuachana na kiungo huyo, suala hilo wamelipeleka na kumwachia Kocha Mkuu mpya, Abdelhak Benchikha kuamua hatima yake ya kubakia au kuondoka, huku ikielezwa kuwa kocha huyo pia huenda akamuondoa kwenye mipango yake.
“Luis hayupo katika mipango ya kocha Benchikha, ni kutokana na kutokuwa katika kikosi chake, tangu amekabidhiwa timu, kucheza na badala yake hakumpa nafasi ya amejikuta akisugua benchi na kukaa jukwaani.
“Hivyo ni ngumu kumbakisha kama kocha kwa viongozi akipendekeza kuachana naye katika dirisha dogo, licha ya ukubwa wa mkataba wake alionao.
“Hivi karibuni baada ya kocha kutua, alifanya kikao na wachezaji na kuwaambia, yupo tayari kuvunja mkataba na mchezaji yeyote atakayeshindwa kuonyesha ushindani bila ya kuangalia ukubwa wa mkataba alionao,” amesema Bosi huyo.
Mtendaji (C.E.O) wa Simba SC, Imani Kajula hivi karibuni alizungumzia hilo kwa kusema kuwa “Hatutakuwa tayari kumuingilia kocha katika jambo lolote ikiwemo usajili, kupanga kikosi, kwani tunaheshimu ubora wake.