Kiungo Mshambuliaji wa Arsenal Bukayo Saka amesaidia kujenga kijji cha Kontena, ambapo waathirika wa tetemeko la ardhi Morocco watakuwa wakiishi.

Winga huyo wa kimataifa wa England, amechangia ujenzi wa makontena 50 sehemu ambayo watu 255 watakuwa wakishi kama makazi yao mapya.

Kwenye kijiji hicho ambacho Saka amesaidia, watu 42 walipoteza maisha, hivyo amejitokeza kusaidia walionusurika akiwa sambamba na mfuko wa hisani wa Big Shoe.

Kufuatia msaada huo, Saka amesema: “Nilishtuka sana niliposikia kuhusu tetemeko la ardhi Morocco.

Kwa muda ambao tukio limetokea, nilitambua msaada unahitajika haraka, nataka kusaidia watu wa Morocco, nimepata njia ya kuwaisaidia, familia zitapata maeneo mazuri ya kuishi baada ya nyumba zao kubomoka, matumaini yangu kwamba familia 84, watoto 89 wataishi kwa amani katika maisha yao ya kila siku.”

Bukayo Saka becomes a nationwide hero in Morocco

Makontena hayo yana sehemu ya kulala, jiko, choo na mabafu ya kuogea, pia umeme utapatikana kwa ajili ya matumizi mengine.

Mwaka jana Saka alichangia operesheni ya watoto 120 huko Nigeria, na hivi karibuni alisapoti waathirika watetemeko la ardhi ilitokea Uturuki.

Saka aliongeza: “Unapoona hali kama hizi watu wanapigania maisha yao, wamepoteza nyumba zao au wapendwa wao, unazidi kutambua kwamba unavyoishi wewe ni baraka tu za Mungu.

Saka si staa pekee mkubwa wa soka ambaye amekuwa akisaidia jamii.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah amekuwa akichangia pesa nyingi kwa ajili ya kusaidia kwao.

Watendaji Serikalini mjitathmini kama mnatosha - Makonda
Namungo FC wavunja ukimya Dirisha Dogo