Utaratibu wa kupata Leseni ya Kimataifa, unamtaka mwombaji kufuata taratibu mbalimbali ikiwemo kuwa na leseni ya Udereva ya daraja lolote lile iliyo hai ya hapa Nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya utaratibu huo iliyochapishwa na ukurasa wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania (Tanzania Road Safety Ambassadors – RSA), umeelekeza kuwa Mwombaji anatakiwa kuipeleka leseni yake ofisi ya Mamlaka ya Leseni (T) TRA kwa ajili ya ukaguzi.

Aidha, chapisho hilo limeelekeza kuwa, baada ya ukaguzi, Mamlaka ya Leseni (T) TRA, itatoa barua rasmi kwenda kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani(T) kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo.

Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itakagua leseni hiyo pamoja na cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) kuthibitisha uhalali wa leseni na cheti hicho cha umahiri.

Baada ya kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo, Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itatoa barua rasmi kwenda Ofisi ya Automobile Association Tanzania ambayo ndiyo asasi pekee hapa nchini yenye Mamlaka ya kutoa leseni za Kimataifa.

Mourinho: Ninatamani Arsenal itwae ubingwa
Makala: Usiwaamini Viumbe hawa 10, ni hatari