Uongozi wa Klabu ya Brentford umeziarifu Klabu za Arsenal na Chelsea zote za London kama zinahitaji huduma ya Mshambuliaji lvan Toney zitatakiwa kulipa kiasi kikubwa cha pesa ili kuipata saini yake dirisha lijalo la majira ya baridi au kiangazi.

Toney mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu huu hajacheza hata mechi moja kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Brentford inataka kumsainisha mkataba mpya lakini bado watamuuza mwisho wa msimu ingawa lazima ofa itakayowasilishwa iwe nono zaidi kwa sababu mabosi wa Brentford wanaamini jamaa ni mmoja kati ya wachezaji watano bora kwa sasa.

Taarifa za ndani zinaeelza Brentford wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 80 Milioni ili kumuuza Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 21 kwenye mechi 25 za michuano yote na Arsenal na Chelsea zinapigana vikumbu kuhakikisha zinanasa saini yake dirisha la Januari 2024.

Try Again: Banchikha atapewa chochote atakacho
Lazima tukiri Umeme ni changamoto - Makonda