Karibu wa itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi – CCM, Paul Makonda amewataka watendaji wa serikali kujitathmini kama nafasi walizopewa zinafanya yale yaliyokusudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kumuwakilisha kwenye kuwahudumia Wananchi.

Makonda ameyaema hayo hii leo Desemba 21, 2023 jijini Dar es salaam wakati akitoa tathmini ya ziara mbalimbali zilizofanywa na viongozi wa CCM ya kuzungumza na wananchi na kujua changamoto zinazowakabili.

Amesema, “hizi ziara tumezifanya kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na tumepata kero nyingi sasa niwaombe watendaji ambao mmewekwa kumsaidia Rais mjitathmini Je? mnafaa kuwepo mlipo na Je? mnatimiza matakwa ya Rais wetu katika kuwahudumia wananchi.”

Katika hatua nyingine, Makonda pia amewataka Wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kwenye dira ya maendeleo ya mwaka 2025/2050, ili kutoa dira kwa Serikali katika upangaji wa shughuli za kimaendeleo.

Majogoro azitoa udenda Pirates, Chiefs
Saka asaidia waathirika Morocco