Katibu wa Itikadi ,Uenezi na Mafunzo Chama cha Mapinduzi – CCM, Paul Makonda amesema tatizo la umeme limekuwa ni changamoto na kuwataka watendaji wa Shirika la umeme nchini – TANESCO, kujitathimini.

Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika hii leo Desemba 21, 2023 jijini Dr es Salaam kwenye Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Lumumba.

Amesema, “hakuna haja ya kutafuna ama kumung’unya maneno ifike mahala lazima kusema ukweli tatizo la umeme limekuwa ni sugu sio tu kwa wananchi wakawaida lakini hata kwa viongozi kwani na wenyewe wanaishi mtaani kama ilivyo wananchi wa kawaida.”

“Watendaji wa Shirika la umeme wanatakiwa kujitathimini, haiwezikani Mwenyekiti hadi analazimika kuvunja hadi Bodi kwasababu uwajibikaji mdogo wa watendaji, kama wameshindwa basi wanatakiwa kujipima,” alisema Makonda.

 

lvan Toney apandishwa thamani England
Kipa Tabora United aisubiri Young Africans