Baadhi ya Raia waliojitokeza kupiga kura mjini Goma, wameshindwa kutekeleza haki yao kimsingi ya kushiriki zoezi hilo kutokana na amuda, wakati huu ambapo zoezi la kuhesabu kura likiwa linaendelea katika baadhi ya vituo vyakupigia kura nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.

Zoezi hilo, limekamilika katika baadhi ya vituo huku hesabu za kura zikiwa zinaendelea huku Mawakala wa wagombea na waangalizi kutoka miungano mbalimbali wakifanya ukaguzi wa majina yalio pigiwa kura.

Hata hivyo, Wananchi waliokosa kushiriki zoezi hilo walijitokeza tena kuitikia wito wa Tume ya Uchaguzi ya Congo – CENI, iliyotangaza kuongeza muda wa siku moja kwa mchakato huo, lakini hawakufanikiwa kwani milango ilikuwa tayari imefungwa.

Baadhi ya wapiga kura pia waliolala nje ya vituo vya kupigia kura, walidai dosari walizozishuhudia zinawapa wasiwasi kuhusu matokeo ya uchaguzi.

Yondani atoa somo Geita Gold
Majanga ya zamani yasipewe kisogo