Beki mkongwe anayeitumikia Geita Gold, Kelvin Yondani amekiangalia kikosi hicho kilivyo kwa sasa katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, kisha kuwaambia wenzake ni lazima wakaze buti na kupambana kiume ili kuhakikisha wanaiokoa timu hiyo isishuke daraja.

Timu hiyo, inayonolewa kwa sasa na Denis Kitambi aliyepokea mikoba ya Hemed Suleiman ‘Morocco’ ipo nafasi ya 11 katika msimamo ikikusanya pointi 16 na jioni ya jana iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate, lakini mapema Yondani amesema wanajipanga kuipigania timu chini ya kocha mpya.

“Ni kweli kila kocha ana mbinu zake, lakini tukiwa na utayari ama ushapu wa kujua kocha anataka kitu gani kwetu, tutaingia kwenye mfumo wake kwa uharaka, hilo litsaidia kufanya vizuri kwenye mechi ambazo zipo mbele yetu,”

“Ligi ni ngumu inahitaji kujitoa kuhakikisha tunashinda mechi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo, vinginevyo huko mbele kunaweza kukawa na mtihani na mahesabu makali.” amesema Yondani

Yondani pia amewataka vijana kuona fursa ya kufanya vizuri kwenye soka, kunavyoweza kuwapa heshima mbele ya jamii, bila kujali wanacheza timu gani.

Young Africans yampigia hesabu Msuva
Uchaguzi DRC: Raia washindwa kupiga kura Goma