Klabu ya ya Manchester United inamtolea macho winga wa zamani wa Real Madrid, Takefusa Kubo kama mbadala wa Antony.

Antony mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Man United kwa Pauni 85.5 milioni, hata hivyo mchango wake kwenye timu ni mdogo tangu alipotua.

Winga huyo wa kimataifa wa Brazili, amefunga mabao manane, asisti tatu katika mechi 62 alizocheza tangu alipojiunga na Mashetani Wekundu.

Na msimu huu, winga huyo ameanza vibaya kwani hajacheka na nyavu katika mechi 18 alizocheza licha ya kupewa nafasi na kocha Erik ten Hag.

Kutokana na kiwango kibovu cha Antony, Ten Hag ameanza kusaka mbadala wake, na tayari wamepeleka maskauti wa kumfuatilia Kubo.

Winga huyo wa kimataifa wa Japan mwenye umri wa miaka 22, amekulia katika kituo cha kukuza vipaji cha La Masia cha FC Barcelona kwa muda wa miaka minne, kabla ya kusajiliwa na Real Madrid mwaka 2019.

Hata hivyo, hakuwahi kuchezea kikosi cha kwanza cha Real Madrid na kutolewa kwa mkopo Mallorca, Villarreal na Getafe, kabla ya kuuzwa Real Sociedad msimu uliopita kwa Pauni 5.5 milioni.

Kutokana na kiwango chake bora, SSC Napoli ilitoa ofa ya Pauni 26 milioni katika dirisha la usajili lililopita, lakini Sociedad ikagoma kumuuza kwa mabingwa hao watetezi wa Serie A.

Kwa sasa klabu hiyo inapanga mikakati ya hatma ya Kubo ambaye mkataba wake utamalizika mwaka 2027 na inaamika kuwa Soeidad itakubali kuumuza winga huyo kwa Pauni 43 milioni.

Malawi yapiga marufuku uagizaji bidhaa toka nje
Simba SC yaanza mazungumzo Nigeria