Imeripotiwa kuwa Klabu ya Arsenal haitaki kumuuza, Eddie Nketiah, wakati wa dirisha la usajili la Januari, huku mshambuliaji mwenyewe akibainika hataki kuondoka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alichezea England kwa mara ya kwanza katika kiwango cha juu Oktoba, mwaka huu anahusishwa na kuhamia katika klabu kadhaa pinzani. Lakini sasa inaeleweka Arsenal haitazamii kuachana na Nketiah.
Hata kama watalazimika kumuuza basi watataka kiasi kinachoweza kufikia Pauni Milioni 50 ambazo ni sawa na zile walizomuuza, Folarin Balogun kwenda AS Monaco msimu wa joto.
Brentford, ambayo imekuwa ikipendekezwa zaidi kutoa ofa huku kukiwa na mustakabali usio na uhakika wa Ivan Toney, bado haijaweka wazi nia yake.
Nketiah amefunga mabao sita na asisti nne katika mechi 23 alizochezea Arsenal msimu huu, ingawa amecheza zaidi ya dakika 60 katika mechi 12 pekee kati ya hizi.
Alimaliza msimu wa 2022/23 akiwa na mabao tisa na asisti tatu katika michezo 39, ingawa tena alitumiwa kwa kiasi na kuelekea mwisho wa michezo kwa sehemu kubwa ya msimu.
Arsenal ilimwongeza Nketiah mkataba utakaodumu hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka, 2027.