Kiungo Mshambuliaji wa Manchester United, Jadon Sancho, anawindwa na klabu za Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen, RB Leipzig na Stuttgart, vyanzo vimethibitisha kwa 90min.

Sancho hajaichezea United tangu Agosti, mwaka huu baada ya kutolewa kwenye kikosi cha kwanza kwa kukosana na kocha, Erik ten Hag.

Kocha huyo alipendekeza winga huyo asijumuishwe kwenye kikosi cha siku ya mechi wakati walipofungwa 3-1 na Arsenal kwa sababu ya kiwango duni alichoonyesha mazoezini, lakini Sancho alikanusha hilo katika mitandao ya kijamii na amekataa kumwomba radhi Ten Hag kwa kosa hilo.

Na sasa timu tatu za Leverkusen, Leipzig na Stuttgart zimeonyesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili Sancho.

Mapema mwezi huu, 90min iliripoti Leipzig inakaribia kumpoteza Fabio Carvalho Januari 2024, huku Liverpool ikitafuta kukatiza mkataba wake wa mkopo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amecheza dakika 360 pekee hadi sasa.

Kwa hiyo Leipzig wako sokoni kwa chaguo jingine la mshanmbuliaji na wanamwangaikia Sancho.

Hata hivyo, mshahara wake mkubwa utafanya mpango wowote kuwa mgumu ikiwa Sancho ataondoka kwa mkopo, United wanataka sehemu nzuri ya mshahara wake kulipwa na wangependelea kujumuisha kifungu cha lazima cha ununuzi.

Gamondi kutumia silaha za Afrika
Ahmed Ally: Tunarudi Ligi Kuu kwa akili kubwa