Polisi nchini Ujerumani, imesema inawashikilia watu 25 wanaosadikika kuwa ni kundi la kigaidi la mrengo wa kulia, wanaoshukiwa kupanga shambulio dhidi ya bunge, ili kuipindua Serikali ya nchi hiyo.
Watu hao wa vuguvugu la raia wa Reichr (Reichsbuerger), wanashukiwa kufanya matayarisho madhubuti ya kulazimisha kuingia katika Bunge la nchi hiyo wakiwa na kundi dogo lenye silaha.
Aidha waendesha mashitaka kwa kushirikiana na Polisi wamesema, washukiwa waliokamatwa ni sehemu ya kundi la kigaidi ambalo lengo lao ni kupindua Serikali iliyopo madarakani.
Hata hivyo, washukiwa walikamatwa katika majimbo ya Ujerumani ya Baden-Wuerttemberg, Bavaria, Berlin, Hesse, Lower Saxony, Saxony, Thuringia na vile vile Austria na Italia na wanatuhumiwa kujiandaa, tangu mwisho wa Novemba 2021, kufanya vitendo hivyo kulingana na itikadi zao.