Johansen Buberwa – Kagera.
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi LaPolisi Mkoani Kagera, kwa tuhuma za vifo vya Watoto saba wa familia moja na majeruhi wanne, ambao walifariki dunia katika kijiji cha Nyakanazi kilichopo Wilayani Biharamlo Mkoani Kagera kwa kile kinachosadikika kuwa walikula chakula chenye sumu.
Vifo hivyo, vilitokea kwa nyakati tofauti baada ya wanafamilia 11 kula chakula cha usiku wa Novemba 13, 2023, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda alisema asubuhi yake watoto watatu walianza kujisikia vibaya wakakimbizwa kituo cha afya Nyakanazi na wakati wanaendelea na matibabu Novemba 14, 2023 wakapoteza maisha.
Aliwataja watoto hao kuwa ni Brayan Ezekiel (2), Kahindi Samson (9) ambaye ni mwanafunzi wa awali shule ya msingi Muungano na Happines Razaro (12) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Muungano na waliofariki kuwa ni Melisiana Razaro (11) na Melina Razaro (9) huku Josephina Juma (5) akiwa alikuwea akiendelea na matibabu.