Kuna ile hali ambayo inakuijia pale unapopata taarifa ya jirani yako au mtu ambaye unamfahamu kuwa amepata mafanikio juu ya jambo fulani, wapo ambaohujisikia vibaya au kubeza au wengine hufurahia na kumuombea heri.
Sina hakika wewe huwa unakuwa upande gani lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba ukitaka kujua kuwa wewe ni mwenye kijicho dhidi ya mafanikio au jitihada za mwenzio, jiulize maswali machache.
1. Unaposikia jirani kanunua Gari, kajenga Nyumba, kaanzisha biashara na mafanikio mengine mengine wewe huwa unajisikiaje moyoni mwako kwa wakati huo?
2. Jirani yako anapokuomba ushauri wa kuanzisha jambo fulani la kimaendeleo iwe kununua shamba au kuanzisha Kampuni huwa unamshauri kwa moyo mweupe au unatoa ushauri usiofaa ili kuvuruga malengo kwa hila?
Bila shaka kwa vyovyote vile majibu ya maswali haya yanatosha kukujulisha wewe binafsi iwapo una HUSDA dhidi ya mafanikio ya mwenzio au la, sasa hebu chukua muda wako na uujifanyie tathmini ili ujijue upo upande gani?
Ikiwa utajikuta una gere, husda na kijicho, basi badilisha mtazamo na ikiwa upo upande wake kwa mfumo chanya usio na hila basi MUNGU azidishe mafanikio katika bidii zako nawe upate matokeo chanya.