Jeshi la polisi Mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa watatu Jenipher Petro (19), Mernrs Petro (22) na Emmanuel Julius (31), wakazi wa Kijiji cha Nyakanazi wakituhumia kuweka dawa za Kienyeji zenye sumu aina Biazion inayotumika kuua wadudu kwenye mboga za majani na kusababisha vifo vya watu saba wa familia Moja na Majeruhi wanne wilayani Biharamulo.

Akizungumza na Vyombo vya Habari hii leo Desemba 23, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Blasius Chatanda amesema watuhumiwa hao wamehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo la kuweka dawa ya sumu kwenye mboga za majani ya Maharage baada ya kumtuhumu familia ya Lazaro Sabakanka kuiba kuku wao mmoja na kwenda kumchinja.

Amesema, “watumia hao walitoroka mara baada ya kutekeleza mauaji Novemba 13, 2023 na kwenda kujificha kwa kaka yao Emmanuel Julius katika kijiji cha Shinyanga A kilichopo kata ya Nayakukuru Wilayani Mbogwe Mkoani Geita>

Hata hivyo, Kamanda CHATANDA ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na Vitendo mabalimbali vya uhalifu ikiwemo mauaji na makosa mengine kuacha mara moja na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote wanaofanya vitendo hivyo vya kiuhalifu ikiwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani.

Nditi aiota Morocco AFCON 2023
Kwa jambo hili wewe upo upande gani?