Dunia imejaa maajabu sana, mengine hayaishii kustaajabisha bali yanakufanya utafakari na hata kukosa majibu, lakini uhalisia unabaki kuwa maajabu yapo.
Ipo hivi, tumezoea kuona Hotel mbalimbali zenye mshangazo lakini kuna moja ipo Nchini Poland katika mji wa Lubrin inajulikana kwa jina la Heaven Hotel.
Hoteli hiyo ina vitanda ambavyo vimejengwa ukutani mwa mwamba wa mlima uitwao Rysy ambavyo huruhusiwa kulala mtu mmoja pekee.
Ukiwa kwenye vitanda hivyo, unaweza kufurahia kuona mandhari ya hadi chini ardhini kupitia vioo vya vitanda hivyo, lakini kuna sharti moja kwamba ukiwa ndani ya vyumba hivyo hutakiwi kula wala kujisaidia.
Wahudumu huelekeza kwamba endapo mteja atataka kujisaidia basi atalazimika kubonya kifaa maalumu kisha Helicopter huja kukuchukua, ili ukajiasaidie na kukurudisha kwenye chumba chako.
Aidha, gharama ya kulala kwenye vitanda hivyo kwa siku ni dola laki 2.5 na hiyo ni kwa mtu mmoja, sasa nawaza mandhari yalivyo na kiasi cha pesa unachotakiwa kulipa, ukijumlisha na uoga, hofu na mengineyo wewe mwenzangu vipi ungelipia ulale?.