Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Kikosi cha usalama barabarani, limeyazuia kuendelea na safari mabasi matano ya abiria katika Stendi kuu jJijini Mbeya baada ya kugaguliwa na kukutwa na changamoto katika mifumo mbalimbali.

Akizungumza hii leo Desemba 26, 2023 Mwanasheria Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Deus Sokoni amesema, katika zoezi hilo jumla ya mabasi 58 yalikaguliwa.

Ameyataja mabasi hayo kuwa ni, Kampuni ya Turu Best, Isamilo Express, Arusha Express, Msigwa na Ahmed, ambayo yanayofanya safari za masafa marefu kwenda mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Afisa leseni wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini – LATRA, Amani Masuwe amesema abiria waliokuwa wanasafiri na mabasi yaliyozuiliwa walipata usafiri mwingine na wengine kurudishiwa nauli zao.

Joshua Kimmich ageuka lulu England
Ahmed Ally: Kutajwa FIFA ni heshima kubwa, tutapambana