Kufuatia matokeo ya sare ya 2-2 ambayo Simba SC waliyapata Jumamosi (Desemba 23) dhidi ya KMC, Kocha mkuu wa Simba SC, Abdelak Benchikha amegeuka mbogo baada ya wachezaji kushindwa kutumia nafasi za wazi ambazo walizitengeneza kupitia mchezo huo.

Simba SC wameshindwa kuibuka na matokeo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi kuu tangu kocha huyo achukuwe mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa, Roberto Oliviera ambaye alitimuliwa.

Kocha Benchikha amesema kuwa hajafurahishwa na wachezaji wake kushindwa kutumia nafasi nyingi ambazo walizitengeneza jambo ambalo limepelekea wameshindwa kupata matokeo ambayo yalikuwa ni ya muhimu zaidi kwao.

“Tulitengeneza nafasi nyingi kakini shida kubwa ilikuwa ni kwa upande wetu wachezaji wangu ambao walishindwa kuzitumia zile nafasi na kuzifanya kuwa mabao, kwa timu kubwa kama Simba SC haiwezi kuwa na furaha na haya matokeo.

“Hii inasababishwa na malengo ya timu yetu kuwa lazima kila msimu tuweze kuubeba ubingwa, sasa kama tutakuwa tunadondosha pointi namna hii hii ni hatari kwetu, tutahakikisha kuwa tunafanya maboresho pale ambapo tumekosea katika michezo iliyopita,” amesema Kocha Benchikha.

Coastal Union kusajili Kenya, Uganda
Atta Agyei: Uongozi Singida FG umenitelekeza