Kiungo na Nahodha wa zamani wa kikosi cha Ivory Coast, Yaya Toure amechagua timu yake anayopigia upatu kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023), michuano itakayofanyika nchini mwake.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester City ameichagua Morocco ambayo ilifika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA 2010 (Afrika Kusini), Senegal na Guinea Bissau kwenda mbali.

Toure ambaye alishinda AFCON mwaka 2015 akiwa na Ivory Coast anaamini timu hizo nne zina uwezo wa kwenda mbali na kutwaa ubingwa kwa kuzingatia ubora wake.

“Nimesema Senegal, Morocco, Guinea Bissau, na Afrika Kusini. Utendaji wao ulikuwa wa kuvutia.”

Toure amesema kuwa Senegal ilitwaa taji la mwisho nchini Cameroon na itamenyana na wenyeji wa mwisho wa michuano hiyo, Guinea na Gambia katika Kundi C.

Morocco ambayo ni timu inayoshika nafasi ya kwanza Barani Afrika kabla ya mashindano hayo itatarajia kutwaa taji lao la pili nchini Ivory Coast baada ya kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia lililopita, ikiwa ni timu ya kwanza ya Afrika kufarikiwa kupata ushindi huo.

Watapambana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia na Tanzania katika Kundi F.

Kwa Guinea Bissau, wenyeji, Ivory Coast, Nigeria na Guinea ya Ikweta wanawasubiri katika Kundi A.

Afrika Kusini ambayo ilishinda AFCON mwaka 1996 na kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010, itacheza na Tunisia, Mali na Namibia katika Kundi E.

Waelezwa umuhimu wa kuyaacha makazi salama
Paza sauti: Simu zisiwaendeshe Madereva