Lydia Mollel-Morogoro.
Wananchi wa mkoa wa Morogoro, wametakiwa kuhakikisha wanaacha makazi yao salama pindi wanapotoka nyumbani na kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.
Hayo yamesemwa na Polisi Kata wa Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro Sajenti, John Simfukwe wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa CCT Forest Kata ya Mkundi Wilaya na Mkoa wa Morogoro, juu ya umuhimu wa kuacha mlinzi/ulinzi katika maeneo yao ili kuzuia wizi na uharibifu wa mali mali zao.
Simfukwe, ametoa elimu hiyo baada ya wananchi hao kulalamika kuwa wanaibiwa mali zao mchana na kushindwa kuwatambua wezi wanaotekeleza uhalifu huo.
Amesema, wazazi walioshindwa kuwalea kimaadili watoto wao kiasi cha kufikia kuwa wadokozi na hata kuwa wezi wawafikishe ofisini kwake lengo likiwa ni kuzungumza nao ili waweze kubadilika la sivyo hatawachukulia hatua za kisheria.
Nao wakazi wa eneo la CCT Forest wamesema mbinu walizopewa na Polisi watazifanyia kazi, ili kuweza kuondokana na wizi unaoendelea kwani ni kero kwenye mtaa wao.