Mabingwa wa Soka Duniani, Klabu ya Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili chipukizi Claudio Echeverri kutoka River Plate ya Argentina, kwa mujibu wa 90min.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 amevutia baadhi ya klabu kubwa Ulaya tangu alipoingia katika kikosi cha kwanza cha River Plate mwaka wa 2023, na kucheza mara sita katika mashindano yote huku wababe hao wa Argentina wakishinda Ligi Kuu ya Argentina.
Kiungo huyo mshanbuliaji alivutia sana katika Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17, akifunga hat-trick maarufu katika ushindi wa Robo Fainali dhidi ya wapinzani wao wakuu Brazil.
90min iliripotiwa mwanzoni mwa Desemba kwamba Man City na Chelsea zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Echeverri, na mchezaji huyo wa zamani sasa anakaribia kukamilisha dili baada ya kuendelea na mazungumzo wiki za hivi karibuni.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kumfanya kijana huyo abaki River hadi angalau msimu wa joto, lakini anaweza kusalia hadi mwisho wa 2024 ili kupata dakika muhimu za kikosi cha kwanza.
Vyanzo vya habari vimethibitisha kwamba Man City wamesonga mbele na mazungumzo, huku pia Chelsea na Barcelona zikimwania.
Pamoja na Echeverri, 90min inaelewa kwamba Man City pia wanavutiwa na vijana wa River Plate Agustin Ruberto na lan Subiabre pia.
Ruberto na Subiabre wote pia walivutia kwenye Kombe la Dunia la U-17 wakiwa na Argentina, huku Ruberto akitwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu kutokana na mabao yake manane mazuri wakati wa mashindano nchini Indonesia.
Wawili hao, kama Echeverri, pia wamevutiwa na sehemu nyingine, huku Brighton and Hove Albion, Tottenham Hotspur, Real Madrid na Barcelona zikiwa kweye mazungurmzo.