Kocha Mkuu wa Asec Mimosas, Julien Chevalier amesema hana kizuizi kwa supastaa wake Karamoko Sankara kujiung na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, lakini litakuwa pigo kwa timu yake.

Young Africans imekuwa ikitajwa kutaka saini ya mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa ameshatupia manne, moja zaidi ya Pacome Zouzoua wa Young Africans.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Ivory Coast amekuwa kwenye ubora wa juu na tetesi zimekuwa zikimhusisha zaidi na Young Africans, ingawa haitaweza kumtumia kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu kwa kuwa ameshaitumikia Asec.

Julien ambaye timu yake imeshafuzu hatua ya Robo Fainali ikitokea Kundi B, ikiwa pamoja na Simba SC, Jwaneng Galaxy na Wydad Casablanca amesema kama ataondoka, basi watakuwa na kipindi kigumu hasa katika michuano ya kimataifa kwani ni mchezaji tegemeo ambaye bado anamuhitaji.

Amesema licha ya kuwa katika nafasi nzuri bado wanahitaji ushindi ambao unaletwa na wachezaji wazuri kama mshambuliaji huyo, lakini uwezekano wa kuondoka unategemea na maamuzi ya uongozi wa klabu.

Asec haizuii mchezaji kuondoka kama kuna timu itakuwa inamtaka, ila kama akiondoka kwa hatua tuliyopo basi tutapoteza mchezaji muhimu ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

“Sisi tuna utaratibu wa kuwaruhusu wachezaji kuondoka kama wanakwenda kupata maslahi mazuri zaidi na huyu pia tunaweza kumruhusu, lakini nilitamani kuona anaondoka mwishoni mwa msimu siyo sasa.

Timu huwa inapitia wakati mgumu mchezaji mkubwa akiondoka, mfano Aziz Ki na Pacome Zouzoua walikuwa bora lakini Young Africans ilipowahitaji basi waliondoka na huyu itakuwa hivyo hivyo,” amesema Julien.

Asec ambayo ilitoka sare ya bao 1-1 na Simba SC kwenye Uwanja wa Mkapa zitakutana tena Februari 23, 2024 nchini Ivory Coast, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambao utaamua hatma ya timu hiyo ya Msimbazi kufuzu au kutofuzu hatua ya Robo Fainali.

Asec imekuwa moja ya timu za Afrika ambayo inawasajili wachezaji wa kiwango cha chini cha fedha na baadae inawauza kwa fedha nyingi bila kujali ni kipindi gani au mchezaji ana umuhimu gani kwenye timu kwa wakati huo.

Vita ya uhalifu: Vijiwe vya Bodaboda kusajiliwa,
Wallace Karia ampongeza Rais Hussein Mwinyi