Mabingwa wa Soka nchini Hispania FC Barcelona wapo tayari kuachana na beki wao, Marcos Alonso dirisha lijalo na mkataba wake utakuwa unamalizika na hawana mpango wa kumwongeza kutokana na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu.

Alonso mwenye umri wa miaka 32, aliwahi kuhusishwa na Man United katika dirisha lililopita lakini dili halikufanikiwa na ikiwa ataachwa huru Erik Ten Hag huenda akavutiwa kumsajili kwa ajili ya kuboresha eneo lake la ulinzi linaloonekana kuwa na mapungufu tangu kuanza kwa msimu.

Awali Barca ilidaiwa kutaka kumuuza Januari mwakani lakini majeraha aliyopata ndio yanaonekana kukwamisha kwani anatarajiwa kupona mwishoni mwa Januari.

Alonso aliwahii kucheza kwa kiwango bora akiwa na Chelsea kuanzia mwaka 2016 hadi 2022, kabla ya kujiunga na Barca kwa usajili huru.

Benchi la ufundi la Barca halijaridhishwa na kiwango chake kwa msimu huu ambapo amecheza mechi nne tu kwenye La Liga.

Makonda ataka ushirikiano endelevu Serikali, Viongozi wa Dini
Vita ya uhalifu: Vijiwe vya Bodaboda kusajiliwa,