Klabu ya Azam FC inadaiwa kukamilisha usajili wa kipa Mohamed Mustafa (27), kutoka Al-Merrikh ya Sudan na huenda akaanza kuonekana kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar.
Mmoja wa viongozi wa Azam ameliambia gazeti hili kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya makipa wao kusumbuliwa na majeraha yatakayowaweka nje muda mrefu.
Wakati makipa Ali Ahamada na Abdullah lddrisu wakiendelea na matibabu, Azam inaamini kipa huyo atakuwa msaada kwenye mechi za Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Mapinduzi.
Kipa huyo alikuwa langoni kwenye michezo miwili ya hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kati ya Yanga na Merrikh ambapo Yanga ilibuka na jumla ya mabao 3-0.
Wakati huohuo, Azam leo inatarajiwa kumtambulisha mshambuliaji wa kati Frankilin Navarro, raia wa Colom- bia aliyetokea klabu ya lorneo ya nchini kwao.