Askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, kutoa elimu kwa jamii, kuwa na matumizi sahihi ya tochi pamoja na kutoa elimu ya sheria za usalama barabarani kwa jamii.
Wito huo, umetolewa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi wakati wa kikao kazi naAskari hao wakilenga kufanya tathmini na kubaini changamoto mbalimbali.
Alisema, jamii inahitaji elimu zaidi ili kuweza kupunguza malalamiko kwa Jeshi la Polisi lakini pia kuzuia ajali za barabarani, huku akisisitiza kutumia busara kwenye maamuzi na kuzingatia matumizi sahihi ya tochi wawapo kazini.
Kwa upande wake Mkuu wa Usalama Barabarani Iringa (SSP) Mossi Ndozero amemshukuru Kamanda kwa kikao hicho na kuahidi kuyasimamia na kuyatekeleza maelekezo yote.