Baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Mtumbuka kutoka Stand United kwa ajili ya kuongeza nguvu upande wa ushambuliaji, klabu ya Mashujaa FC iko kwenye hatua ya mwisho ya kuwasajili wachezaji Mapinduzi Balama na Abdul Makame ‘Bui’.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa viongozi wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kuwasajili wachezaji hao kwa mkataba wa miezi sita kwanza ili kuangalia viwango na ufanisi wao wa kazi, kabla ya kuwaongeza miaka miwili kama watafanya vyema.

Balama anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na Bui ambaye ni kiungo mkabaji, wote wawili wameshawahi kuitumikia klabu ya Young Africans.

Balama ni mmoja wa wachezaji walioachana na Coastal Union katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Msemaji wa Klabu hiyo, Hamisi Milyango amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao huku wakikamilisha usajili Mtumbuka.

“Tumemsajili mwamba, Mshambuliaji wa boli, Mtumbuka kutoka Stand United, jamaa anafunga mabao na kutengeneza ‘assist’ kweli kweli.

Benchikha: Kila mchezaji Simba SC atacheza
Athumani jela miaka 35 kwa ubakaji, kuambukiza virusi