Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta anadaiwa kuwasilisha jina la beki wa Bayern Munich, Matthijs de Ligt kwenye ripoti ya mastaa ambao anataka wasajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya baridi kwa ajili ya kuboresha eneo lake la ulinzi, ambalo licha ya kufanya vizuri kwa msimu huu bado linaonekana kuhitaji mabadiliko.

De Ligt mwenye umri wa miaka 24 ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora kwa msimu huu na inaonekana kuwa ni vigumu Bayern kumuuza kutokana na umuhimu wake kwenye timu.

Pamoja na Bayern Munich kutoonekana kwamba inahitaji kumuuza kuna uwezekano ikabadilisha uamuzi au timu inayomhitaji itatoa kiasi cha zaidi ya Pauni 70 milioni.

De Ligt alijiunga na Munich kwa ada ya uhamisho ya Pauni 68 milioni mwaka jana akitokea Juventus, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Tangu kuanza kwa msimu huu, amecheza mechi 11 za michuano yote na kufunga bao moja.

Chama awekwa sokoni kwa Dola 300,000
Benchikha: Kila mchezaji Simba SC atacheza