Mshambuliaji mpya wa Geita Gold, Ramadhan Kapera amefurahia kujiunga na kikosi hicho huku akiahidi kufanya makubwa kama alivyofanya akiwa na timu ya Mbeya Kwanza ya Ligi ya Championship aliyoachana nayo dirisha hili dogo.

Kapera amesema licha ya kuanza maisha yake mapya na kikosi hicho ila hana presha yoyote kwani ana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu Bara, hivyo anachoomba ni sapoti ya mashabiki na wachezaji wote ili wafikie malengo yao.

“Ni furaha kwangu kujiunga hapa ila ni changamoto pia kwa sababu kiwango bora nilichoonyesha Mbeya Kwanza ndicho ambacho kimewavutia mabosi wa Geita kunisajili, naamini kwa kushirikiana na wenzangu tutafanya vizuri zaidi ya sasa,” amesema.

Kwa upande wa aliyekuwa Kocha wa Mbeya kwanza Maka Mwalwisi amesema usajili wa Kapera utaisaidia sana Geita kutokana na uhodari wa nyota huyo kwenve kufunga huku akiamini kama atapewa nafasi.

Usajili huo ni wa kwanza kwa Kocha wa Geita, Denis Kitambi aliyependekeza kuongezewa nguvu katika eneo la ushambuliaji msimu huu pekee, nyota huyo amefunga mabao tisa katika michezo 14 akiwa na Mbeya Kwanza.

Serikali kujenga kituo cha Afya eneo lililotengwa Hanang'
Mbombo anaondoka Azam FC