Imefahamika kuwa Azam FC muda wowote watakamilisha dili la usajili la Mshambuliaji Reliants Lusajo aliyetangaza kuachana na Namungo FC.

Lusajo mwanzoni mwa juma hili kupitia moja ya kurasa zake za mitandao ya kijami, aliandika ujumbe wa kuwaaga Viongozi na Mashabiki wa Namungo FC katika usajili huu wa dirisha dogo msimu huu 2023/24.

Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC imefikia makubaliano mazuri na Lusajo ya kumpa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo na atambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ya chamazi, baada ya kila kitu kikikamilika.

“Ni suala la muda pekee kwa Azam FC kumtambulisha Lusajo, baada ya kufikia muafaka mzuri na Azam FC baada ya kuachana na waajiri wake wa zamani Namungo FC.

“Lusajo ameandaliwa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Azam FC, hivyo muda wowote atasaini na kutambulishwa akijiunga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Namungo FC,” amesema mtoa taarifa hizi.

Ofisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe amezungumzia usajili wa Mshambuliaji huyo kwa kusema: “Wapo wachezaji wengi wanaotajwa Azam FC, lakini kama uongozi tunazungumzia usajili uliokamilika pekee.”

Baraza: Muda utaisaidia Dodoma Jiji
Wanaume acheni mawazo hasi - Dawati la Jinsia