Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Galatasaray, Wilfried Zaha, ameachwa na Kocha Jean-Louis Gasset, katika kikosi cha wachezaji 27 cha Ivory Coast kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.
Mchezaji huyo alihamia katika Ligi Kuu Uturuki kutoka Crystal Palace mwishoni mwa msimu uliopita, ameichezea Ivory Coast mechi mbili pekee za kirafiki mwaka huu na kukosa mechi za kufuzu AFCON na mzunguko wa kwanza wa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwezi uliopita.
Gasset amewajumuisha Serge Aurier wa Nottingham Forest, Ibrahim Sangare, na Willy Boly pamoja na kiungo wa kati wa Al-Ahli Franck Kessie na winga wa Trapzonspor Nicolas Pepe, ambaye anarejea baada ya kukosekana kwa mwaka mmoja.
Ismael Diallo wa Hajduk Split aliitwa kwa mara ya kwanza, huku Lazare Imani wa Union Saint Gilloise akiunda kikosi chake cha pili.
Washambuliaji Sebastien Haller wa Borussia Dortmnund na Karim Konate wa RB Salzburg pia wapo kwenye kikosi hicho ambacho ni wenyeji, kitamenyana na Guinea-Bissau katika mchezo wa kwanza Januari 13, 2024.
Pia watacheza dhidi ya Nigeria na Equatorial Guinea katika Kundi A.
Kikosi kamili: Makipa – Yahia Fofana (Angers SCO), Badra Ali Sangare (Sekhukhune United) na Charles Folly (ASEC Mimosas)
Walinzi: Serge Aurier (Nottingham Forest), Wilfried Singo (AS Monaco), Obite Ndicka (AS Roma), Ousmane Diomande (Sporting CP), Odilon Kossonou (Baye Leverkusen), Willy Boly (Nottingham Forrest) na Ghislain Konan (Al-Fayha).
Viungo: ldrissa Doumbia (Al-Ahli Doha), Franck Kessie (Al-Ahli), Sangare (Noting Michael Seri (Hull City) na Lazare Amani ham Forest), Seko Fofana (AI Nassr), Jean Michael Seri (hull City) na Simon Adingra (Brighton & Hove Albion).
Washambuliaji: Nicolas Pepe (Trapzonspor), Max-Alain Gradel (Gaziantep), Karim Konate (RB Salzburg), Sebastien Haller (Borussia Dortmund), Oumar Diakite (Stade Reims), Jonathan Bamba (Celta Boga (Jecemie), Christian Kouame (Fiorentina) na Jean-Philippe Krasso (Belgrade).