Klabu ya LAFC iko katika mazungumzo ya kumsajili Mlinda Lango wa Tottenham Hotspur, Hugo Loris kutua kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), kwa mujibu wa ESPN.
Mchezaji huyo mwenye umnri wa miaka 37 yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Spurs na Kocha Ange Postecoglou hajamchezesha hata dakika moja.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mpango huo umekamilika na kukubaliwa kabla ya kukamilishwa na kuna uwezekano hakutakuwa na ada ya uhamisho inayohusika.
Spurs ilimsajili Guglielmo Vicario kutoka Empoli kwa ada ya Pauni Milioni I7.2 Juni, mwaka huu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia haraka akajitambulisha kama kipa chaguo la kwanza la Postecoglou.
Lloris alikuwa huru kuondoka katika majira ya joto lakini alikataa ofa za Lazio, Nice na klabu za Ligi Kuu Saudi Arabia.
Kipa huyo wa zamani wa Ufaransa alijiunga na Spurs akitokea Lyon mwaka wa 2012 na baada ya vita vifupi vya kutafuta nafasi ya kuanza katika timu hiyo akiwa na kipa Brad Friedel, alifanikiwa kuwa nambari namba moja katika timu hiyo ya London Kaskazini.
Lloris alichezea Spurs zaidi ya mechi 400, akiteuliwa kuwa nahodha msimu wa 2015-16 na aliyekuwa kocha wa wakati huo Mauricio Pochettino, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Son Heung-Min muda mfupi baada ya Postecoglou kuchukua usukani.
Alitwaa Kombe la Dunia kama nahodha wa Ufaransa mwaka 2018 kabla ya kustaafu soka la kimataifa Januari, mwaka jana akiwa ameichezea mechi 145.