Jeshi la Polisi nchini, limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja ambayo aliyafanya Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjro Novemba 12, 2023 kisha kukimbia.

Akitoa taarifa hiyo hii leo Desemba 31, 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo leo Desemba 31, 2023 walifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo.

Amesema, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha akjaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu lakini walifanikiwa kumuwahi na kumkimbiza kituo cha afya kupata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.

Hata hivyo, Misime amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

 

Sherehe zisiwasahaulishe mahitaji ya Watoto Shuleni - Maganga
TAMWA ZNZ yahimiza upunguzaji malalamiko ya udhalilishaji