Wazazi wa Kata ya Nyangao Wilayani na Mkoa wa Lindi, wametakiwa kukumbuka kuandaa mahitaji muhimu ya Wanafunzi wakati huu wa kuelekea kufunguliwa kwa shule zote nchini ifikapo Januari 8, 2024.
Hayo ameyasema Polisi wa Kata wa Kata ya Nyangao, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Andrew Maganga wakati alipojumuika na wananchi hao kwenye sherehe ya kimila maarufu Unyago iliyofanyika Desemba 30, 2023.
Amesema, miezi ya kuelekea mwisho wa mwaka sherehe huwa ni nyingi na zinagharimu mahitaji makubwa jambo linalopelekea wazazi wengi kutojiandaa na mahitaji muhimu ya wanafunzi pale shule zinapokuja kufunguliwa mpaka kushindwa kuwapeleka watoto shule.
Aidha, mewatahadharisha kujiandaa kwa siku chache zijazo kwani Serikali inamtaka kila mzazi kumpeleka mtoto shule ambapo atakayeshindwa aweze kuchukuliwa adhabu ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kupelekwa mahakamani.