Lydia Mollel – Morogoro.
Katika hatua za kupambanba na kutokomeza kabisa uhalifu,biashara haramu na utumiaji wa dawa za kulevya jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kukamata mifuko 30 ya dawa za kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa kg. 430 Kijiji na kata ya Mangae Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro kwenye zikiwa gari lenye namba za usajiri T.301 DPG na tela namba T.562 DNV Lori, Kampuni ya K.T. Abri.
Akiongea na Vyombo vya Habari katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP. Alex Mkama ameeleza kuwa hadi sasa bado wanamtafuta Dereva aliehusika kwani ametelekeza gari hilo baada ya kushtukia mtego wa Polisi.
Amesema, pia Jeshi la polisi linawatafuta waendesha pikipiki 6 walitoroka na kutelekeza pikipiki zao baada ya kushtukia mtego wa Polisi katika Kijiji cha Mangae kata ya Mangae Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Disemba 31, 2023.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi katika kijiji cha Kimamba B’ wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro limemkamata Ahmad Salum Mlali miaka 31, Mkulima mkazi wa Kimamba B akiwa na miba 256 ya Nungunungu pamoja na bunduki mbili Aina ya Shotgun na Rifle zikiwa na maganda 71 ya risasi.
Mtuhumiwa anatumia bunduki hizo katika shughuli za Uwindaji haramu kwenye Hifadhi zilizopo jirani ambapo Kamanda Mkama ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Jeshi la Polisi lizifanyie kazi kwa haraka na kuleta hali ya ushwari katika mkoa huu.
Itakumbukwe kuwa ndani ya Desemba, 2023 vitendo mbalimbali vya kiuhalifu katika Mkoa wa Morogoro vimeendelea kudhibitiwa katika Misako iliyofanyika, ili kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kudumishwa.