Baada ya Arsenal kuyumba kwa siku za karibuni ndani ya Premier League, imeripotiwa kwamba, kocha wa timu hlyo, Mikel Arteta, amepanga kuingia sokoni kipindi hiki cha usajilil wa dirisha dogo ili kuimarisha kikosi chake.
Arsenal ambayo katika Sikukuu za Krismasi 2023 ilikuwa kileleni mwa msimamo wa Premier, imejikuta ikianguka hadi nafasi ya nne siku ya mwisho ya mwaka 2023.
Hiyo imetokana na kushindwa kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo, ikimalizia kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Fulham. Kabla ya hapo, ilitoka 1-1 dhidi ya Liverpool, kisha ikafungwa nyumbani 0-2 na West Ham.
Katika mipango yao ya usajili, imeripotiwa a kwamba, Arsenal inavutiwa na huduma ya Victor Osimhen ambaye ndani ya Napoli, ili kumnyakua kwa sasa timu inatakiwa kutoa Pauni 120m.
Tatizo kubwa ambalo linaonekana ndani ya Arsenal ni uhaba wa kufunga mabao, mpaka sasa timu hiyo imefunga mabao 37 katika Premier, matatu kutoka kwa Mshambuliaji wao namba moja, Gabriel Jesus. Kwa upande wa Eddie Nketiah, amefunga matano.
Arsenal imekuwa pia ikihusishwa na usajili wa Mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney, ambaye alikuwa amefungiwa kwa makosa ya kujihusisha na kamari, msimu uliopita alifunga mabao 20 katika Prermier League.