Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Party cha Korea Kusini, Lee Jae-myung ameshambuliwa kwa kuchomwa kisu shingoni na mtu asiyejulikana.
Shambulio hilo, lilitokea wakati Lee alipokuwa akikagua eneo lililopendekezwa kwa ujenzi wa uwanja mpya wa Ndege huko Busan mapema asubuhi ya leo hii Januari 2, 2023 ambapo mshambiliaji huyo awali alitaka saini ya Kiongozi huyokama ishara ya kumkubali lakini alikuwa na nia tofauti.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 59 alipokea matibabu ya dharura katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pusan mjini Busan na kisha kuhamishiwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Seoul kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 67, amekamatwa na Wahudumu wa afya wanasema mshipa wa kubeba damu kutoka kichwani kwenda moyoni wa Bwana Lee umeathiriwa kutokana na kuvuja kwa damu nyingi.