Tetemeko kubwa la ardhi lililofikia kipimo cha 7.6 katika jimbo la Ishikawa lilisababisha mawimbi ya tsunami yenye urefu wa zaidi ya mita moja huku moto mkubwa ukilipuka na kuharibu barabara, ambapo mpaka sasa Watu 57 wamepoteza maisha.
Uharibifu mkubwa ulitokea katika eneo la Noto ambapo majengo yaliharibiwa na moto, nyumba kubomoka, boti za uvuvi kuzama au kusombwa ufukweni, na barabara kuu kuharibiwa kufuatia maporomoko ya ardhi.
Hata hivyo, Shirika la habari la JapanKyodo limeripoti watu walokufa huenda ikaongezeka kutokana na uhalisia wa tukio na kwamba shughuli za uokozi bado zinaendelea ili kuwapata manusura.
Nchi hiyo, mwaka 2011 pia iliwahi kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa 9.0 kipimo cha Richter, ambalo lilisababisha tsunami na kupelekea vifo vya watu 18,500.