Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe, Mrakibu wa Polisi Jane Warioba amefanya ukaguzi wa magari ya kubeba Wanafunzi ambao wanatarajia kufungua shule hivi karibuni.
Warioba amefanya ukaguzi huo hii leo Januari 3, 2024 na kuwataka madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani pindi wanapokuwa wamepakia Wanafunzi wa shule, ili kuweza kupunguza matukio ya ajali.
Hatua hiyo pia imechykuñiwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara ambalo pia limefanya ukaguzi wa Magari ya shule ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka kabla ya Muhula wa masomo kuanza, ili kubaini changamoto mbalimbali za magari hayo na kutoa maelekezo ya matengenezo kwa yake yatakayobainika kuwa na kasoro.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya Posta Manispaa ya Musoma, Mkuu wa Kikosi cha usalama rarabarani Mkoa wa Mara, Mrakibu wa Polisi Mathew Ntakije alisema lengo la ukaguzi huo ni kuweka mazingira salama kwa wanafunzi wanaotumia magari hayo.