Klabu ya Chelsea inahusishwa na mpango wa kuanza mchakato wa kuwania saini ya beki kisiki wa Nice, Jean Clair Todibo anayewindwa pia na Manchester United na Tottenham Hotspur.
Todibo mwenye umri wa miaka 24, ameonyesha kiwango bora tangu msimu uliopita na kuzivutia timu nyingi Barani Ulaya ingawa Manchester United ndio inapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini yake kutokana na uhusiano mzuri wa Nice na bosi mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford, Sir Jim Ratcliffe.
Chelsea ina tatizo kwenye safu ya ulinzi na inamuona nyota huyu kuwa sahihi kwenda kuimarisha eneo hilo na mwisho wa msimu beki wao kiongozi, Thiago Silva ataondoka pia.
Mkataba wa sasa wa Todibo utamalizika ifikapo 2027 na inadaiwa ili kumpata Todibo itahitajika zaidi ya Pauni 7O milioni.
Beki huyu wa kati kwa sasa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu lakini msimu huu amecheza mechi 14 za Ligi Kuu Ufaransa na kutoa asisti moja.