Mshambuliaji wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris St-Germain, Kylian Mbappe bado amesema hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.

Mkataba wa nahodha huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 na mabingwa hao wa Ligue 1 unamalizika mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa kuhamia Real Madrid.

Juni mwaka jana, Mbappe aliiambia PSG kwamba hataongeza mkataba mwingine baada ya alionao kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Kwanza kabisa, nina ari sana, sana, sana kwa mwaka huu. Ni muhimu sana)” alisema

Mbappe mara baada ya mechi yao na Toulouse ambao waliwachapa mabao 2-0 na kutwaa taji la Mabingwa wa Ufaransa.

“Kama nilivyosema, tuna mataji hilo tayari limefanyika. Baada ya hapo, hapana, sijafanya uamuzi bado.

Lakini kwa vyovyote vile, kwa makubaliano niliyofanya na mwenyekiti Nasser Al-Khelaifi msimu huu wa joto, haijalishi ninaamua nini.

Tulifanikiwa kulinda pande zote na kuhifadhi utulivu wa klabu kwa changamoto zinazokuja, ambayo inasalia kuwa jambo muhimu zaidi.”

Mbappe alijiunga na PSG mwaka wa 2017, awali kwa mkopo kutoka AS Monaco.

Gamondi ahimiza usajili wa Mshambuliaji
Bodaboda waishitaki Serikali kwa kutoshirikishwa mipango